Leo hii, uwekezaji sio tena kitu cha watu wenye uzoefu pekee. Kwa kutumia teknolojia, kila mtu anaweza kuanza kuwekeza kwa urahisi na ufanisi zaidi. Hii sehemu itakufundisha jinsi ya kutumia vifaa vya kidijitali kufanikisha mipango yako ya kifedha – bila riba, bila mizigo, na kwa uhakika wa matokea.
Soko la hisa sio tena la "watu wa kwenye ofisi" – sasa unaweza kufuatilia na kuwekeza kutoka popote!
DSE HISA KIGANJANI ni programu ya simu (Android & iOS) inayokupa:
✔ Bei za sasa za hisa na hati fungani
✔ Taarifa za kampuni (faida, madeni, gawio)
✔ Uchambuzi wa mwenendo wa soko
✔ Kufanya maagizo ya ununuzi/uuza kupitia madalali
Pakua App kutoka Google Play Store au App Store.
Jisajili kwa kutumia namba yako ya simu.
Chagua madalali (kama VFSL) kwa usaidizi wa moja kwa moja.
Anza kufuatilia na kuwekeza!
🔸 KISHAURI CHA VFSL:
"Usiogope kujaribu! Anza kwa kufuatilia hisa 3-5 kwa wiki moja, halafu wekeza kwa ujasiri."
Ni akaunti ya kielektroniki ambayo:
✔ Inahifadhi hisa na hati fungani zako kwa njia salama.
✔ Inakuwezesha kupokea gawio na mavuno moja kwa moja.
✔ Inarahisisha uhamishaji wa mali bila karatasi.
Tembelea Benki Au Dalali (kama VFSL).
Jaza Fomu na weka taarifa zako (NIDA, picha, taarifa za benki).
Pata Namba Yako Ya CDS baada ya usajili.
Anza Kuwekeza!
⚠️ MAHITAJI YA MSINGI:
Kitambulisho halali (NIDA/Passport)
Picha passport-size
Akaunti ya benki
Nunua hisa kwa urahisi kupitia:
✔ M-Pesa (Lipa kwa madalali)
✔ NMB Mobile, CRDB Mkononi
✔ Mifumo kama Mixx by Yas
TradingView – Kuchambua ramani za hisa kwa urahisi.
Bloomberg Terminal (Kwa wataalamu) – Taarifa za soko la kimataifa.
DSE Website – Taarifa rasmi za soko.
VFSL Blog – Uchambuzi wa soko na mbinu.
Hakuna haja ya:
❌ Kukaa benki kwa masaa kusajili hati fungani.
❌ Kutembelea DSE kila siku kufuatilia bei.
❌ Kuchanganyikiwa na mambo ya karatasi.
Teknolojia imebadilisha kila kitu!
✔ Anza kuwekeza leo hata kwa TZS 10,000.
✔ Fuatilia mali yako kwa simu yako.
✔ Pata mavuno bila riba kwa urahisi.
ChuoSmart Notifications
Stay updated with the latest products, courses, and messages by enabling notifications.