Kozi ya lugha ya Kichina kwa Kiswahili – Kutoka Mwanzo hadi Kuelewa

Kozi ya lugha ya Kichina kwa Kiswahili – Kutoka Mwanzo hadi Kuelewa

Free Course
General Course

Course Modules

Viewing Preview

You can view this course without enrolling. Your progress won't be saved unless you login and enroll.

You're previewing this course. Login to enroll to save your progress.

Malengo:

  • Kujua matamshi ya Kichina (Pinyin).

  • Kujitambulisha na kutumia salamu za kawaida.

Somo:

Kichina Pinyin Matamshi kwa Kiswahili Maana
你好 Nǐ hǎo Nii hao Habari / Hello
您好 Nín hǎo Nin hao Habari (kwa heshima)
谢谢 Xièxiè She-she Asante / Thank you
对不起 Duìbuqǐ Dwei-bu-chi Samahani / Sorry
Qǐng Ching Tafadhali / Please
我叫… Wǒ jiào … Wo jiao … Jina langu ni… / My name is…

Mazoezi:

  • Jitambulisho: “Nǐ hǎo, Wǒ jiào [jina]”

  • Fanya mazoezi ya matamshi ya Pinyin kila siku (A, O, E, I, U, Ü).

No content available for this module yet.

Malengo:

  • Kujua namba 1–20 na rangi kuu.

  • Kujua vitu vya nyumbani na mahali.

Somo:

Namba:

Kichina Pinyin Matamshi Maana
yii Moja / 1
èr aa-r Mbili / 2
sān saan Tatu / 3
sii Nne / 4
uu Tano / 5
liù liou Sita / 6
chii Saba / 7
baa Nane / 8
jiǔ jiu Tisa / 9
shí shii Kumi / 10

Rangi:

Kichina Pinyin Matamshi Maana
hóng hong Nyekundu / Red
lán lan Bluu / Blue
绿 liu Kijani / Green
bái bai Nyeupe / White

Vitu vya nyumbani:

Kichina Pinyin Matamshi Maana
桌子 zhuōzi zhuo-zi Meza / Table
椅子 yǐzi yii-zi Kiti / Chair
mén men Mlango / Door
shuǐ shuei Maji / Water
食物 shíwù shii-wu Chakula / Food

Mazoezi:

  • Hesabu vitu nyumbani kwa Kichina.

  • Eleza rangi na vitu ulivyoona.


No content available for this module yet.

Malengo:

  • Kujenga sentensi rahisi.

  • Kuuliza na kujibu maswali ya kila siku.

Somo:

Kichina Pinyin Matamshi Maana
我去学校 Wǒ qù xuéxiào Wo chü shue-siao Ninaenda shule / I go to school
我喜欢吃 Wǒ xǐhuān chī Wo shii-huan chi Ninapenda chakula / I like eating
什么时候? Shénme shíhou? Shen-me shihou Ni lini? / When?
哪里? Nǎlǐ? Na-li Wapi? / Where?
Shì Shi Ndiyo / Yes
不是 Bù shì Bu shi Hapana / No

Mazoezi:

  • Tengeneza sentensi zako za kila siku: “Ninaenda sokoni”, “Ninapenda kahawa”.

  • Jaribu kuuliza maswali kwa Kichina.

No content available for this module yet.

Malengo:

  • Kujieleza hisia.

  • Kutumia alama kueleza mahali na muda.

Somo:

Kichina Pinyin Matamshi Maana
高兴 Gāoxìng Gao-shing Furaha / Happy
伤心 Shāngxīn Shang-shin Huzuni / Sad
生气 Shēngqì Sheng-chi Hasira / Angry
这里 zhèlǐ Je-li Hapa / Here
那里 nàlǐ Na-li Pale / There
今天 jīntiān Jin-tien Leo / Today
明天 míngtiān Ming-tien Kesho / Tomorrow
昨天 zuótiān Zwo-tien Jana / Yesterday

Mazoezi:

  • Eleza hisia zako au tukio kwa Kichina.

  • Tumia alama kueleza mahali na muda.

No content available for this module yet.

1. Muundo wa Kawaida wa Sentensi

Sentensi nyingi za Kichina zinafuata Mfumo wa SVO (Subject + Verb + Object), sawa na Kiswahili na Kiingereza.

Mfano:

  • 我吃苹果。

  • Wǒ chī píngguǒ.

  • Mimi nakula tofaa.

Ufafanuzi:

  • 我 (Wǒ) = Mimi (subject)

  • 吃 (chī) = Kula (verb)

  • 苹果 (píngguǒ) = Tofaa (object)


2. Kutumia Viashiria vya Wakati (Time)

Kichina kinatumia viashiria vya wakati mwanzoni au kati ya subject na verb ili kuelezea wakati wa kitendo.

Mfano:

  • 我今天去学校。

  • Wǒ jīntiān qù xuéxiào.

  • Mimi leo ninaenda shule.

Ufafanuzi:

  • 今天 (jīntiān) = Leo

  • Muundo: Subject + Time + Verb + Object

Mifano ya viashiria vingine vya wakati:

  • 昨天 (zuótiān) – Jana

  • 明天 (míngtiān) – Kesho

  • 现在 (xiànzài) – Sasa


3. Kutumia Viashiria vya Mahali (Place)

Mahali huzungushwa na viashiria kabla ya kitenzi au mwisho wa sentensi.

Mfano:

  • 我在家吃饭。

  • Wǒ zài jiā chī fàn.

  • Mimi nikipika/nikila chakula nyumbani.

Ufafanuzi:

  • 在 (zài) = katika / iko

  • 家 (jiā) = Nyumbani

  • 吃饭 (chī fàn) = Kula chakula

Muundo: Subject + Place + Verb + Object


4. Kuunda Maswali

a) Maswali ya Ndiyo/Hapana:
Ongeza 吗 (ma) mwishoni mwa sentensi.

  • 你好吗?

  • Nǐ hǎo ma?

  • Unaendeleaje? (Ndiyo/Hapana)

b) Maswali ya Taarifa:
Tumia maneno ya kuuliza kama:

  • 什么 (shénme) – Nini

  • 谁 (shéi) – Nani

  • 哪里 (nǎlǐ) – Wapi

  • 什么时候 (shénme shíhou) – Lini

Mfano:

  • 你吃什么?

  • Nǐ chī shénme?

  • Unakula nini?


5. Kutumia Negation (Hapana / Si)

  • 不 (bù) – kwa sasa/future tense, si / hapana

  • 没 (méi) – kwa past tense, hakuna

Mfano:

  • 我不喝水。

  • Wǒ bù hē shuǐ.

  • Sishingi maji / Si ninakunywa maji

  • 我没吃早饭。

  • Wǒ méi chī zǎofàn.

  • Sijala kiamsha kinywa


6. Kutumia Conjunctions (Na, Au, Lakini)

  • 和 (hé) = na

  • 还是 (háishì) = au

  • 但是 (dànshì) = lakini

Mfano:

  • 我喜欢苹果和香蕉。

  • Wǒ xǐhuān píngguǒ hé xiāngjiāo.

  • Ninapenda tofaa na ndizi

  • 你喝茶还是咖啡?

  • Nǐ hē chá háishì kāfēi?

  • Unakunywa chai au kahawa?


7. Tipi Rahisi za Kutunga Sentensi za Kila Siku

  1. Subject + Verb + Object

    • 我喝水。 Wǒ hē shuǐ – Ninakunywa maji

  2. Subject + Time + Verb + Object

    • 我今天去学校。 Wǒ jīntiān qù xuéxiào – Leo ninaenda shule

  3. Subject + Place + Verb + Object

    • 我在家吃饭。 Wǒ zài jiā chī fàn – Nikila nyumbani

  4. Question (Ndiyo/Hapana)

    • 你好吗? Nǐ hǎo ma? – Unaendeleaje?

  5. Question (Taarifa)

    • 你吃什么? Nǐ chī shénme? – Unakula nini?

No content available for this module yet.

1. Pinyin ni nini?

  • Pinyin ni mfumo wa kuandika matamshi ya Kichina kwa herufi za Kilatini.

  • Kila herufi ina sauti maalumu, tofauti na Kiswahili kidogo.

  • Matamshi yanahusiana sana na tones (midundo).


2. Tones (Midundo)

Kichina kina midundo 4 muhimu (+ tone isiyo na midundo):

Tone Alama Mfano Matamshi kwa Kiswahili
1 ¯ Maa (sauti inabaki juu, ndogo)
2 ˊ Ma (sauti inaenda juu, kama kuuliza)
3 ˇ Ma (sauti inashuka kisha juu)
4 ˋ Ma (sauti inashuka haraka)
5 / Neutral ma Ma (sauti haina nguvu, ya kawaida)

Mfano:

  • 妈 (mā) – Mama

  • 麻 (má) – Hemp / mmea

  • 马 (mǎ) – Farasi

  • 骂 (mà) – Kukasirishwa

Mazoezi:

  • Jitafute neno moja na useme kwa tones zote.

  • Sikiliza audio kwenye apps kama HelloChinese au Yoyo Chinese.


3. Vowels (Sauti za Kimsingi)

Pinyin Matamshi kwa Kiswahili Mfano
a aa 爸 (bà) – Baba
o o 我 (wǒ) – Mimi
e e 了 (le) – Tayari / Kumaliza
i i 你 (nǐ) – Wewe
u u 书 (shū) – Kitabu
ü iu / yu 绿 (lǜ) – Kijani

Mazoezi:

  • Sema kila vowel kando na tone.

  • Jaribu maneno rahisi kama mā, mǎ, mà, má.


4. Consonants (Sauti za Mwanzo)

Kichina kina baadhi ya consonants ambazo hazipo Kiswahili, zingatia hizi rahisi:

Pinyin Matamshi kwa Kiswahili Mfano
b b 爸 (bà) – Baba
p p (na pumzi kidogo) 跑 (pǎo) – Kukimbia
m m 妈 (mā) – Mama
f f 飞 (fēi) – Kuruka
d d 大 (dà) – Kubwa
t t (na pumzi kidogo) 天 (tiān) – Mbingu
n n 你 (nǐ) – Wewe
l l 老 (lǎo) – Mzee
g g 狗 (gǒu) – Mbwa
k k (na pumzi) 开 (kāi) – Fungua
h h 好 (hǎo) – Nzuri
j j 鸡 (jī) – Kuku
q ch (laini) 去 (qù) – Kwenda
x sh (laini) 谢 (xiè) – Asante

Mazoezi:

  • Chagua neno rahisi na sema consonant + vowel + tone.

  • Sikiliza audio ili kuiga matamshi.


5. Muundo Rahisi wa Kutamka Maneno

  1. Chukua consonant + vowel → sema polepole

  2. Ongeza tone → fanya kama ilivyo kwenye tone table

  3. Rudia maneno mara 3–5 hadi midundo iende sawa

Mfano:

  • 你 (nǐ) → n-i + tone 3 (shuka kisha juu)

  • 好 (hǎo) → h-a-o + tone 3 (shuka kisha juu)

  • 你好 (Nǐ hǎo) → rudia polepole 3x, kisha jaribu kuzungumza kama kawaida


6. Mazoezi ya Kila Siku

  • Sema salamu 5–10 kila siku kwa tones sahihi.

  • Sikiliza audio kwenye apps au YouTube na jaribu kuiga maneno.

  • Andika Pinyin kisha usome kwa sauti.

  • Changanya consonant + vowel + tone kwa maneno tofauti.

No content available for this module yet.

Quizzes & Assessments

No assessments have been created for this course yet.

Instructors

  • Captain
    +255659256606

Course Information

  • Course Type General Course
Chat with us!
Home Shop Blog Jobs Cart Search
ChuoSmart ChuoSmart Notifications

Stay updated with the latest products, courses, and messages by enabling notifications.