Katika ulimwengu wa kisasa wa kidijitali, mashambulizi ya mtandao yamekuwa ya kawaida na hatari zaidi. Ili kujilinda, kuna hatua muhimu ambazo kila mtumiaji wa kompyuta au simu anapaswa kuchukua kila siku.
Programu hizi husaidia kugundua na kuzuia virusi na malware kabla hayajaleta madhara.
Sasisha (update) antivirus yako kila wakati.
Hakikisha programu hiyo ina uwezo wa kuchunguza barua pepe, tovuti na faili unazopakua.
Watu wengi huambukizwa virusi au malware kupitia barua pepe au jumbe za mitandaoni (WhatsApp, Telegram, SMS) zenye viungo vya hatari.
Usibofye link au kufungua faili kutoka kwa mtu usiyemfahamu au hata mtu unayemjua ikiwa ujumbe unaonekana wa kushangaza.
Hata ukipokea ujumbe kutoka kwa namba ya kawaida unaokuomba utume namba ya kadi au nywila – jua ni ulaghai.
Manenosiri dhaifu hufanya akaunti zako kuwa rahisi kuvunjwa (hacked).
Tumia mchanganyiko wa herufi kubwa, ndogo, namba na alama (mf. E$ema2025!).
Usitumie nywila moja kwa akaunti zote.
Badilisha nywila zako mara kwa mara.
Wahalifu wa mtandao hutumia mapungufu (vulnerabilities) ya mifumo isiyosasishwa.
Weka Windows, Android, iOS, MacOS n.k. zikiwa updated.
Pia hakikisha unafanya updates za apps zako.
Kupakua programu au kutembelea tovuti zisizo salama ni hatari.
Pakua apps/programu kutoka kwenye vyanzo rasmi tu kama Play Store, App Store au tovuti rasmi ya kampuni.
Usitembelee tovuti za “filamu bure”, “cracked software”, au “beti ya bure” ambazo mara nyingi hubeba virusi.
Mitandao ya bure kama ya hoteli, ofisi, au stendi za mabasi si salama.
Usifungue akaunti zako za benki, au kufanya miamala ukiwa kwenye Wi-Fi ya umma.
Ikiwezekana, tumia VPN unapounganishwa kwenye Wi-Fi ya watu wengine.
Mashambulizi mengi huanza kwa mtu kujifanya kama mfanyakazi wa benki, kampuni ya simu, au taasisi fulani.
Kamwe usitoe taarifa binafsi kwa simu au ujumbe hadi uthibitishe unazungumza na nani.
Wasiliana na taasisi kupitia namba rasmi – si namba uliyotumiwa kwa ujumbe.
Hii ni njia ya kuongezea ulinzi zaidi kwenye akaunti zako.
Baada ya kuingiza nywila, unatumiwa namba ya siri (OTP) kwenye simu yako ili kuthibitisha ni wewe.
Hii huzuia mtu mwingine kuingia hata kama amepata nywila yako.
Kama kompyuta au simu yako inafanya kazi polepole sana, au inaonekana kuna apps mpya hujapakua — chunguza mara moja.
Hakikisha unajua kila app au programu iliyo kwenye kifaa chako.
Usalama wa kidijitali ni jukumu la kila mtu. Elimisha familia yako, wanafunzi, au wafanyakazi wenzako kuhusu:
Hatari za kushiriki nywila
Ujumbe wa ulaghai
Umuhimu wa kutumia vifaa salama
Usalama wa taarifa zako unategemea sana tahadhari zako binafsi. Mashambulizi ya mtandao yanabadilika kila siku, lakini kwa kufuata hatua hizi, unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kudukuliwa au kuathiriwa.
“Usisubiri hadi shambulizi litokee – chukua hatua sasa.”
ChuoSmart Notifications
Stay updated with the latest products, courses, and messages by enabling notifications.