You can view this course without enrolling. Your progress won't be saved unless you login and enroll.
What is a computer
Types of computers (desktop, laptop, tablet)
Parts of a computer (hardware vs software)
CPU (processor)
RAM (memory)
Hard disk / SSD
Keyboard, mouse, monitor, printer
What is an operating system
Windows basics
File and folder management
Installing and uninstalling programs
Creating documents
Formatting text (font, size, bold, alignment)
Inserting images and tables
Saving and printing files
Introduction to spreadsheets
Basic formulas (SUM, AVERAGE, COUNT)
Creating tables and charts
Managing data
Creating presentations
Using templates and themes
Adding images, animations, and transitions
Presenting slides
What is the internet
Using browsers (Chrome, Edge, Firefox)
Creating and using email (Gmail, Outlook)
Online safety basics
Viruses and malware
Antivirus software
Safe browsing habits
Password protection
Proper typing posture
Finger placement
Typing speed and accuracy practice
Basic graphic design (Canva)
Introduction to coding
Cloud storage (Google Drive, OneDrive)
Basic troubleshooting
No content available for this module yet.
Kompyuta ni mashine ya kielektroniki inayopokea taarifa (input), kuzichakata (process), kuzihifadhi (store), na kutoa majibu au matokeo (output).
Kompyuta hutumika kuandika nyaraka, kuvinjari mtandao, kutuma barua pepe, na kutumia programu mbalimbali.
Kompyuta ya Mezani (Desktop)
Hii ni kompyuta inayotumika sehemu moja bila kuhama. Hutumika sana ofisini, shuleni na majumbani.
Kompyuta Mpakato (Laptop)
Ni kompyuta ndogo inayobebeka. Ina skrini, keyboard na betri, hivyo inaweza kutumika mahali popote.
Kompyuta Kibao (Tablet)
Ni kompyuta ndogo yenye skrini ya kugusa (touch screen). Hutumika kwa kuangalia video, kusoma na kutumia mitandao ya kijamii.
Hizi ni sehemu halisi za kompyuta unazoweza kuzishika.
Mfano:
Monitor (Kioo cha kuonyesha picha)
Keyboard (Ubao wa kuandikia)
Mouse (Kipanya)
CPU (Ubongo wa kompyuta)
Printer (Mashine ya kuchapisha)
Hizi ni programu zinazofanya kompyuta ifanye kazi. Huzionekani kwa kushika.
Mfano:
Windows
Microsoft Word
Excel
Vivinjari vya mtandao (browsers)
Kompyuta ni mashine ya kielektroniki inayochakata taarifa. Zipo aina tofauti za kompyuta kama desktop, laptop na tablet. Kompyuta ina hardware (vifaa halisi) na software (programu).
No content available for this module yet.
CPU (Central Processing Unit) ni ubongo wa kompyuta.
Hufanya kazi ya kuchakata taarifa na kutoa maamuzi.
Kadiri CPU ilivyo na kasi kubwa, ndivyo kompyuta inavyofanya kazi kwa haraka zaidi.
RAM ni kumbukumbu ya muda mfupi ya kompyuta.
Huhifadhi programu na kazi zinazotumika kwa wakati huo.
RAM nyingi = kompyuta hufanya kazi haraka
RAM ndogo = kompyuta kuwa polepole
RAM hupoteza taarifa mara kompyuta inapozimwa.
Hii ni sehemu ya kuhifadhi taarifa za kudumu.
Hard Disk (HDD):
Hutumia disk inayozunguka
Ni polepole kuliko SSD
SSD (Solid State Drive):
Haina sehemu zinazozunguka
Ni ya kisasa na ya haraka zaidi kuliko HDD
Huhifadhi:
Mafaili
Picha
Video
Programu
Keyboard (Ubao wa kuandikia):
Hutumika kuingiza maandishi na amri
Mouse (Kipanya):
Hutumika kusogeza mshale kwenye skrini
Kubofya, kuchagua na kufungua vitu
Monitor (Kioo cha Kompyuta):
Huonyesha picha, maandishi na video
Printer (Kichapishi):
Huchapisha maandishi au picha kwenye karatasi
CPU ni ubongo wa kompyuta, RAM ni kumbukumbu ya muda, Hard Disk/SSD hutunza taarifa za kudumu, na vifaa kama keyboard, mouse, monitor na printer hutumika kuingiza na kutoa taarifa.
No content available for this module yet.
Mfumo wa uendeshaji (Operating System – OS) ni programu kuu inayosimamia kazi zote za kompyuta.
Huunganisha kati ya mtumiaji na vifaa vya kompyuta (hardware).
Mifano ya mifumo ya uendeshaji:
Windows
macOS
Linux
Android
Desktop: Skrini kuu ya kompyuta
Start Menu: Mahali pa kufungua programu
Taskbar: Upau wa chini unaoonyesha programu zinazoendelea kufanya kazi
Icons: Alama za programu na mafaili kwenye desktop
Matumizi ya msingi:
Kufungua programu kwa kubofya mara mbili (double click)
Kutumia mouse kusogeza mshale
File (Faili): Hati au taarifa iliyohifadhiwa (mfano: document, picha, video)
Folder: Mahali pa kuhifadhi mafaili pamoja.
Mambo ya msingi:
Kuunda folder mpya: Right click → New → Folder
Kuunda faili mpya: Right click → New → File/Document
Kubadilisha jina: Right click → Rename
Kufuta: Right click → Delete
Kuhamisha: Drag and drop
Kuweka programu (Install):
Pakua programu kutoka mtandao au tumia disk/flash
Fungua file la setup
Fuata hatua (Next → Next → Install → Finish)
Kuondoa programu (Uninstall):
Fungua Control Panel au Settings
Chagua “Apps” au “Programs”
Chagua programu → Uninstall
Thibitisha kufuta
Mfumo wa uendeshaji ndio unaoendesha kompyuta. Windows ina sehemu kuu kama Desktop, Start Menu na Taskbar. Mafaili na folder husimamiwa kwa kuunda, kufuta, na kuhamisha. Programu huwekwa (install) na kuondolewa (uninstall) kupitia mipangilio ya kompyuta.
No content available for this module yet.
Microsoft Word ni programu ya kuandika na kuandaa nyaraka.
Hatua za kuanza:
Fungua Microsoft Word
Chagua Blank Document
Anza kuandika maandishi yako
Hii husaidia kufanya maandishi yaonekane vizuri.
Vipengele vya msingi:
Font: Aina ya herufi (mfano: Times New Roman, Arial)
Size: Ukubwa wa maandishi (mfano: 12, 14, 16)
Bold (B): Kuweka maandishi manene
Italic (I): Kuweka maandishi ya kuegemea
Underline (U): Kuweka mstari chini ya maandishi
Alignment:
Left (kuanza kushoto)
Center (katikati)
Right (kulia)
Justify (kulinganisha pande zote)
Kuingiza picha:
Bonyeza Insert → Pictures
Chagua picha kutoka kompyuta → Insert
Kuingiza meza (Table):
Bonyeza Insert → Table
Chagua idadi ya mistari (rows) na safu (columns)
Kuhifadhi (Save):
Bonyeza File → Save As
Chagua mahali pa kuhifadhi (Desktop, Documents, Flashdisk)
Andika jina la faili → Save
Kuchapisha (Print):
Bonyeza File → Print
Chagua printer
Bonyeza Print
Microsoft Word hutumika kuandika nyaraka. Inawezesha kurekebisha maandishi, kuingiza picha na meza, na kuhifadhi au kuchapisha mafaili.
No content available for this module yet.
Microsoft Excel ni programu ya kutengeneza na kusimamia taarifa katika mfumo wa jedwali.
Workbook: Faili kubwa ya Excel
Worksheet (Sheet): Ukurasa mmoja ndani ya workbook
Row (Safu ya mlalo): Mistari ya kulala (1, 2, 3…)
Column (Safu ya wima): Mistari ya kusimama (A, B, C…)
Cell: Sehemu moja ya kuingiza data (mfano: A1, B2)
Formulas hutumika kufanya mahesabu kiotomatiki.
SUM (Jumla):
Hujumlisha namba.
Mfano:
=SUM(A1:A5)
AVERAGE (Wastani):
Hupata wastani wa namba.
Mfano:
=AVERAGE(A1:A5)
COUNT (Kuhesabu):
Huhesabu idadi ya seli zenye namba.
Mfano:
=COUNT(A1:A5)
Kutengeneza Table:
Andika data zako kwenye seli
Chagua data → Bonyeza Insert → Table
Kutengeneza Chart:
Chagua data
Bonyeza Insert → Chagua aina ya chart (Column, Bar, Pie)
Faida ya charts:
Huonyesha taarifa kwa picha
Hufanya takwimu zieleweke kirahisi
Sorting: Kupanga data kwa herufi au namba
Filtering: Kuchuja data ili kuonyesha taarifa maalum
Editing: Kubadilisha, kuongeza au kufuta data
Freezing panes: Kuweka vichwa vya columns visiwe vinapotea unaposogeza chini
Microsoft Excel hutumika kuhifadhi na kuchambua data. Inatumia formulas kama SUM, AVERAGE na COUNT, hutengeneza tables na charts, na kusaidia kusimamia data kwa urahisi.
No content available for this module yet.
Microsoft PowerPoint ni programu ya kutengeneza maonesho ya slaidi.
Hatua za kuanza:
Fungua Microsoft PowerPoint
Chagua Blank Presentation
Bofya New Slide kuongeza slaidi mpya
Andika kichwa cha habari (Title) na maudhui (Content)
Templates na Themes hutumika kupangilia muonekano wa slaidi.
Bonyeza Design
Chagua theme unayoipenda
Badilisha rangi, fonti na mitindo ya slaidi
Faida:
Wasilisho huonekana la kuvutia na la kitaalamu
Kuingiza picha:
Bonyeza Insert → Pictures
Chagua picha kutoka kwenye kompyuta
Animations (Harakati za maandishi/vitu):
Chagua maandishi au picha
Bonyeza Animations
Chagua aina ya animation mfano: Fade, Fly In
Transitions (Mabadiliko kati ya slaidi):
Bonyeza Transitions
Chagua aina ya mabadiliko ya slaidi
Bonyeza Slide Show → From Beginning
Tumia mishale ya keyboard kubadilisha slaidi
Tumia laser pointer au mouse kuonyesha sehemu muhimu
Microsoft PowerPoint hutumika kutengeneza wasilisho la slaidi. Inawezesha kutumia templates, kuingiza picha, animations, transitions, na kuwasilisha slaidi kwa njia ya kitaalamu.
No content available for this module yet.
Intaneti ni mtandao mkubwa wa kompyuta unaounganisha mamilioni ya kompyuta duniani.
Hutumika:
Kutafuta taarifa
Kutuma na kupokea barua pepe
Kutazama video, kusikiliza muziki, na mitandao ya kijamii
Kufanya biashara na mawasiliano
Vivinjari hutumika kuvinjari intaneti. Mfano maarufu:
Google Chrome
Microsoft Edge
Mozilla Firefox
Mambo ya msingi:
Andika URL au tafuta kwenye search bar
Bonyeza linki kufungua tovuti
Tumia tabs kufungua tovuti nyingi kwa wakati mmoja
Hifadhi favorites/bookmarks kwa tovuti unazotembelea mara kwa mara
Kujenga akaunti ya barua pepe:
Chagua mtoa huduma: Gmail, Outlook, Yahoo
Jaza taarifa za jina, username na password
Thibitisha akaunti kupitia nambari ya simu au barua nyingine
Kutumia barua pepe:
Kutuma barua: New → Andika email → To: (mpokeaji) → Subject → Send
Kupokea barua: Inbox → Soma
Kujibu barua: Reply
Kushirikisha faili: Attach files
Usishiriki password na mtu yeyote
Epuka kubofya links zisizo za kawaida
Tumia antivirus na firewall
Hakikisha websites ni salama (https://)
Intaneti ni mtandao mkubwa wa kompyuta unaowawezesha watu kupata taarifa, kuwasiliana na kufanya biashara. Vivinjari vinasaidia kuvinjari mtandao, wakati barua pepe hutumika kwa mawasiliano rasmi. Usalama mtandaoni ni muhimu kila wakati.
No content available for this module yet.
Virus (Virusi): Programu ndogo inayosababisha kompyuta kushindwa au kudhuru data.
Malware (Programu hatari): Programu yoyote hatari inayoweza kuiba taarifa, kuharibu mfumo, au kusababisha matatizo kwenye kompyuta.
Dalili za virusi/malware:
Kompyuta inakosa kufanya kazi vizuri
Files zinapotea au hubadilika
Programu zinazofungwa bila sababu
Antivirus ni programu zinazotambua na kuondoa virusi na malware.
Programu maarufu: Avast, Kaspersky, Norton, Windows Defender
Vipengele vya msingi:
Scan ya kompyuta
Real-time protection (kinga ya mara kwa mara)
Updates za mara kwa mara
Epuka kubofya links zisizo za kawaida
Usishiriki taarifa binafsi kwenye tovuti zisizo salama
Hakikisha websites zina https://
Usipakue files zisizo halali au zisizo salama
Tumia password yenye mchanganyiko wa herufi kubwa, ndogo, namba na alama maalumu
Usitumie neno linalojulikana (mfano: jina lako)
Badilisha password mara kwa mara
Usishirikishe password yako na mtu mwingine
Usalama wa kompyuta ni muhimu kulinda data na mfumo wako. Programu hatari kama virusi na malware zinaweza kuharibu kompyuta. Antivirus, tabia salama za mtandao, na ulinzi wa nenosiri huweka kompyuta yako salama.
No content available for this module yet.
Kaa wima au wima kidogo kando ya meza
Miguu iwe imesogea ardhini kwa usawa
Miguu na mikono isipishane sana
Usifanye pressure kubwa kwenye keyboard
Angalia skrini bila kukunja shingo sana
Tumia home row keys kama msingi:
Vidole vya mkono wa kushoto: A, S, D, F
Vidole vya mkono wa kulia: J, K, L, ;
Vidole vidogo vya kushoto/vikia vyote vinashika Z, X, C, V na vidole vidogo vya kulia vinashika M, , . /
Vidole vinarudi kwenye home row baada ya kubofya kila herufi
Anza polepole ukizingatia usahihi zaidi ya kasi
Fanya mazoezi ya kila siku ya dakika 10–15
Tumia programu au tovuti za mazoezi ya kuandika
Onyesha maendeleo kwa kupima words per minute (WPM)
Lenga kupunguza makosa mara kwa mara
Typing skills huongeza ufanisi wa kazi za kompyuta. Nafasi sahihi ya mwili, vidole kwenye keyboard, na mazoezi ya kila siku husaidia kuongeza kasi na usahihi wa kuandika.
No content available for this module yet.
Canva ni programu rahisi ya kubuni picha, poster, na mitandao ya kijamii
Hutumia templates tayari
Unaweza kuongeza maandishi, icons, picha na rangi
Hufanya kazi bila ujuzi mkubwa wa picha
Coding ni lugha ya kuandika programu ambazo kompyuta zinaweza kuelewa
Lugha rahisi za kuanzia: HTML, CSS, Python
Hutumika kuunda websites, apps, au automation
Mfano:
Hutoka kwenye idea kuu hadi kutekeleza kazi moja kwa moja kwa kompyuta
Google Drive na OneDrive hutoa nafasi ya kuhifadhi faili mtandaoni
Faida: faili ziko salama, unaweza kuzifikia popote na wakati wowote
Jambo muhimu: weka folders na files vizuri ili urahisi wa kupatikana
Kuzima na kuwasha kompyuta upya (Restart)
Kukagua plugs na kebo
Kutumia Task Manager kuangalia programu zinazokimbia polepole
Ku-update software na antivirus mara kwa mara
Advanced Computer Skills hutoa ujuzi zaidi wa ubunifu, coding, kuhifadhi kwenye wingu, na kutatua matatizo madogo ya kompyuta. Hii inasaidia kuongeza ufanisi na kujua kutumia teknolojia kwa kiwango cha juu.
No content available for this module yet.
| Shortcut | Kazi |
|---|---|
| Ctrl + C | Nakili (Copy) |
| Ctrl + X | Kata (Cut) |
| Ctrl + V | Bandika (Paste) |
| Ctrl + Z | Rudisha kitendo (Undo) |
| Ctrl + Y | Rudisha tena kitendo (Redo) |
| Ctrl + A | Chagua yote (Select All) |
| Alt + Tab | Badilisha kati ya windows |
| Windows + D | Onyesha Desktop |
| Windows + L | Lock screen / Funga kompyuta |
| Ctrl + Shift + Esc | Fungua Task Manager |
| Shortcut | Kazi |
|---|---|
| Ctrl + B | Andika manene (Bold) |
| Ctrl + I | Andika kwa kuegemea (Italic) |
| Ctrl + U | Andika mstari chini (Underline) |
| Ctrl + S | Hifadhi faili |
| Ctrl + P | Chapisha faili |
| Ctrl + F | Tafuta maneno ndani ya waraka |
| Ctrl + Home | Nenda mwanzo wa waraka |
| Ctrl + End | Nenda mwisho wa waraka |
| Shortcut | Kazi |
|---|---|
| Ctrl + C | Nakili (Copy) |
| Ctrl + X | Kata (Cut) |
| Ctrl + V | Bandika (Paste) |
| Ctrl + Z | Rudisha kitendo (Undo) |
| Ctrl + Y | Rudisha tena kitendo (Redo) |
| Ctrl + A | Chagua yote (Select All) |
| Ctrl + Arrow Key | Nenda mwishoni mwa data kwenye direction ya arrow |
| F2 | Hariri seli iliyochaguliwa |
| Ctrl + Shift + L | Washa au zima filter |
| Shortcut | Kazi |
|---|---|
| Ctrl + M | Ongeza slaidi mpya |
| F5 | Anza slideshow kutoka mwanzo |
| Shift + F5 | Anza slideshow kutoka slaidi ya sasa |
| Ctrl + D | Nakili slaidi iliyochaguliwa |
| Ctrl + S | Hifadhi kazi |
| Ctrl + P | Tumia pointer au kuchora kwenye slaidi |
| Ctrl + Shift + C | Nakili formatting |
| Ctrl + Shift + V | Bandika formatting |
No content available for this module yet.
No assessments have been created for this course yet.
ChuoSmart Notifications
Stay updated with the latest products, courses, and messages by enabling notifications.