Hatua za Kufuatilia Cheti Kilichopotea

C By Captain
May 1, 2025
Hatua za Kufuatilia Cheti Kilichopotea

Andika Taarifa ya Kupoteza (Loss Report) Polisi

  • Nenda kituo cha polisi chochote.

  • Eleza kuwa umepoteza cheti chako.

  • Utapewa RB (Report Book) number au loss report kama uthibitisho rasmi.

2. Weka Tangazo la Kupotea kwenye Gazeti

  • Chapisha tangazo fupi kwenye gazeti la kitaifa (mfano: Mwananchi, HabariLeo).

  • Eleza jina lako kamili, aina ya cheti, mwaka wa kuhitimu, na kwamba kimepotea.

3. Andaa Barua ya Maombi ya Nakala Mbadala

  • Iandikwe kwenda kwa Katibu Mtendaji wa Baraza husika (NECTA au NACTE au TCU).

  • Taja jina lako, namba ya mtihani, shule na mwaka uliomaliza.

  • Eleza kuwa umepoteza cheti na unaomba duplicate.

4. Ambatanisha na Barua:

  • Nakala ya tangazo la gazeti.

  • RB (loss report) kutoka polisi.

  • Kitambulisho chako (NIDA au kura).

  • Passport size moja au mbili.

  • Malipo ya ada ya duplicate certificate (kwa NECTA ni TZS 20,000).

5. Wasilisha kwa Baraza Husika:

  • Kama ni NECTA: Wapelekee makao makuu (Dar es Salaam) au ofisi za NECTA za kanda.

  • Kama ni NACTE/TCU kwa vyuo: Wasiliana na chuo husika pia kwa uthibitisho wa kwanza.

6. Subiri Majibu

  • NECTA huchukua wiki kadhaa hadi miezi 2.

  • Watakupa nakala halali (official copy) ya cheti chako.

 

Chat with us!
Home Blog Talents Cart Search
ChuoSmart ChuoSmart Notifications

Stay updated with the latest products, courses, and messages by enabling notifications.